Tuesday, September 3, 2019

UBA TANZANIA YALENGA KUPUNGUZA TATIZO LA VITABU KWA KUGAWA VITABU VYA FASIHI SHULE ZA SEKONDARI TABATA DAR ES SALAAM

  UBA Tanzania wakikabidhi vitabu vya fasihi kwa mkuu wa shule ya sekondari Ugombolwa Simon Machia pamoja na Afisa Mtendaji kata Eligius Mulokozi na wanafunzi wa shule hiyo siku benki ya UBA ilipotembelea kwaajili ya kugawa vitabu hivyo
Asupya Nalingigwa, mkuu wa kitengo cha Digital Banking akikabidhi vitabu kwa wanafunzi wa shule ya Migombani sekondari siku benki ya UBA Tanzania ilipotembelea shule hizo zilizopo Tabata Jijini Dar es salaam

 Mkuu wa kitengo cha Digital Banking kutoka UBA Tanzania, alikimkabidhi vitabu makamu mkuu wa shule ya sekondari ya Zawadi, Dativa Ngowi, siku walipotembelea shule za sekondari Tabata na kugawa vitabu vya Fasihi


Mkuu wa kitengo cha Digital Banking, Asupya Nalingiwa akitoa mawaidha kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Ugombolwa, juu ya umuhimu wa usomaji vitabu siku UBA Tanzania walipotembelea  shule za Tabata jijini Dar es Salaam na kugawa vitabu vya Fasihi
                                                        xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

 UBA Tanzania, siku ya Ijumaa ilitembelea shule mbalimbali za Sekondari za serikali zilizopo Tabata jijini Dar es salaam nakugawa vitabu vya fasihi simulizi kama moja ya njia za kupunguza tatizo la upungufu wa vitabu kwenye shule mbalimbali za Tanzania hasa za serikali.

Shule ambazo zimeangukiwa na neema hiyo ni pamoja na shule ya sekondari ya ugombolwa,Miombani na shule ya sekondari ya Zawadi. Vitabu mbalimbali viligawiwa vikiwemo Things fall apart, The fishermen, The girl that can pamoja na Fine Boy kutoka kwa waandishi maarufu kamavile Chinua Achebe na Chigozie Obioma.


UBA Tanzania imekua mstari wa mbele katika kusaidia ukuaji wa elimu Tanzania kwa kugawa vitabu kwenye shule za sekondari pamoja na kuwezesha miundombinu mbalimbali katika sekta ya elimu.


Akiongea na wanafunzi hao, Asupya Nalingigwa mkuu wa kitengo cha digitali, aliwaambia wanafunzi faida za usomaji vitabu badala ya kujikita zaidi na mambo yasiyo ya muhimu kwenye mitandano ya kijamii.


 Aidha amewashauri wanafunzi kutumia mitandao hiyo kwa kujisomea Zaidi na kujifunza mambo yenye tija.

Mkuu wa shule ya Ugombolwa  Simon Machia ameshukuru msaada uliotolewa na UBA Tanzania na kuwasihi wanafunzi kutumia vitabu hivyo kwa makini na kuongeza ufahamu ili benki ione faida iliyotokana na kupokea vitabu hivyo.


Uongozi wa shule za Miombani na Zawadi pia wamefurahishwa na ugawaji wa vitabu hivyo na kusema kuwa benki haikua na upendeleo na imewaona hata wao ambao shule zao bado zinajikokota ili kufikia malengo na kupanda ngazi kimkoa au kitaifa.


Mbali na uhitaji wa vitabu walimu wakuu hao wameeleza kuwa kuna mahitaji mengine mbalimbali kama vile upungufu wa madarasa ya kusomea, Viti, Meza, Madawati, Komputa pamoja na uzio wa shule ili kuboresha usalama.

Monday, September 2, 2019

Elumelu Challenges Japan – “Partner with us in Empowering African Entrepreneurs”

Achim Steiner, UNDP Administrator Praises Tony Elumelu’s Private-Sector Led Approach         to African Development

·              >President of South Africa, H.E. Cyril Ramaphosa: “If you want really good returns, as Tony        Elumelu said, come to Africa”

>Elumelu Champions Job Creation in Africa at Breakfast Meeting with President of Rwand and UNICEF Executive Director

Tokyo, Japan, August 29, 2019

In an impassioned keynote speech, delivered before global leaders, at the 7th Tokyo International Conference on African Development (TICAD) in Yokohama, Japan, African investor and philanthropist Tony O. Elumelu CON, challenged the Government of Japan to invest 5% of its $50billion commitment to Africa, in empowering African entrepreneurs.

“At TICAD 2016 in Kenya, Japan pledged $30billion for Africa. This year you have generously increased this to $50 billion. If we invested just 5% in Africa’s new generation of entrepreneurs, following my Foundation’s robust, proven model of getting capital directly to those best placed to catalyse growth and create real impact, we could touch 500,000 lives, across the 54 African countries, broadening markets, facilitating job creation, improving income per capita, and laying the key foundation for political and economic stability”, said Mr. Elumelu.

Mr. Elumelu’s statement captured his vision of a relationship between Japan and Africa, which prioritises economic and shared prosperity. He outlined the three key pillars of a bold and transformative structure: investment in infrastructure, partnership with the African private sector, and investment in Africa’s youth.
He urged Japan to learn from the example of the Tony Elumelu Foundation, which champions empowering African entrepreneurs, as the most sustainable means of accelerating the development of Africa. The Tony Elumelu Foundation, in just five years has assisted over 7,500 African entrepreneurs across every African country, with seed capital, capacity building, mentorship and networking opportunities through its $100 million Entrepreneurship Programme.

Elumelu’s advice carried the weight of his track record of business success, founding Africa’s global bank, United Bank for Africa (UBA), which has grown its presence to 20 African countries, as well as in the United Kingdom, France, and the USA; and Heirs Holdings, Africa’s private investment company which actively invests in key sectors of Africa’s economy and controls millions of dollars in its investment portfolio. Together, they employ over 30,000 people and transform the communities they operate in.

“Africa is one of the world’s viable destinations for investment. Our huge population, of nearly 1.3 billion people, creates one of the most attractive markets anywhere in the world. The world is paying close attention to Africa, but is Japan at the centre of this conversation or is it on the sidelines?” he queried.

Mr. Elumelu’s philosophy has become increasingly popular on the African continent, where he is acknowledged as the pioneer of a private-sector-led approach to accelerating development. He repeated the message at the Generation Unlimited breakfast meeting with H.E. Paul Kagame, President of Rwanda and UNICEF Executive Director, Henrietta Fore, with its focus on job creation in Africa, where he emphasised the role the African youth plays in this narrative.

President of South Africa and Co-Chair, TICAD, H.E. Cyril Ramaphosa corroborated Mr. Elumelu’s stance. He said: “If you want really good returns, as Mr. Tony Elumelu said, come to Africa. Africa presents risk-adjusted returns and is a market in which investments are flowing at a hundred billion dollars - that is the new profile of Africa that is being presented to the world.”
Achim Steiner, UNDP Administrator praised Tony Elumelu's Private-Sector led approach to development in Africa. He said: "I want to refer to my dear friend and colleague Tony Elumelu because he alluded to the vital role that business can also play in investing in the future of the youth. These are the kinds of partnerships that will drive business and development agenda to very different heights in the future".
Speaking on the potential of the African continent, Prime Minister Shinzō Abe of Japan said: "In Africa, some countries have joined top nations in the ranking on the ease of doing business. The scale of the market continues to expand. We can envision a day when the entire continent of Africa becomes an enormous economic zone."

Organised by the Japanese Government, TICAD is a three-yearly forum for advancing Africa’s development through people, technology, and innovation, bringing together government, business leaders, companies and other stakeholders. The event hosted Presidents and private sector leaders including Prime Minister Shinzō Abe of Japan; H.E. Mr. Muhammadu Buhari, President of Nigeria; H.E. Mr. Abdel-Fattah El-Sisi, President of Egypt and Chair of the African Union (AU); H.E. Mr. Cyril Ramaphosa, President of South Africa; and H.E. Mr. Paul Kagame, President of Rwanda and a host of other African Presidents.

Monday, May 27, 2019

SERIKALI YAJIPANGA KUUNGANISHA GESI ASILIA MAJUMBANI NCHI NZIMA



Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), Dkt. Raphael Chegeni (katikati), akizungumza jambo wakati wa Semina iliyoandaliwa na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kwa Kamati hiyo kuhusu mchango wa sekta ya gesi na mafuta katika uchumi, Dodoma, Mei 25, 2019. Kushoto ni Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani na kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Mhandisi Kapuulya Musomba.



Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akizungumza wakati wa Semina iliyoandaliwa na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kwa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) kuhusu mchango wa sekta ya gesi na mafuta katika uchumi, Dodoma, Mei 25, 2019.



Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akizungumza wakati wa Semina iliyoandaliwa na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kwa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) kuhusu mchango wa sekta ya gesi na mafuta katika uchumi, Dodoma, Mei 25, 2019.



Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Mhandisi Kapuulya Musomba akiwasilisha Mada kuhusu mchango wa sekta ya gesi na mafuta katika uchumi, wakati wa semina kwa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), iliyofanyika Dodoma, Mei 25, 2019.



Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), ambaye pia ni Mbunge wa Muleba Kaskazini, Charles Mwijage akichangia hoja, wakati wa semina kwa Wabunge wa Kamati hiyo, kuhusu mchango wa sekta ya gesi na mafuta katika uchumi, Dodoma, Mei 25, 2019.



Sehemu ya Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), wakifuatilia mada mbalimbali katika Semina kuhusu mchango wa sekta ya gesi na mafuta katika uchumi, Dodoma, Mei 25, 2019.



Sehemu ya Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), na wataalamu kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), wakifuatilia mada mbalimbali katika Semina kuhusu mchango wa sekta ya gesi na mafuta katika uchumi, Dodoma, Mei 25, 2019.
                                    xxxxxxxxxxxxxxxxxx
 
Na Veronica Simba - Dodoma
Serikali imesema Mradi wa kuunganisha gesi asilia majumbani ni endelevu na utafanyika katika mikoa yote nchi nzima awamu kwa awamu.
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani, alibainisha hayo jana, Mei 25, 2019 jijini Dodoma katika Semina ya Wabunge wa Kamati ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) ambayo ililenga kuwajengea uelewa kuhusu mchango wa sekta ya gesi na mafuta katika uchumi wa nchi.
Akifafanua, Waziri aliwaeleza wabunge hao kuwa usambazaji wa gesi asilia majumbani umeanza katika Mikoa mitatu ya mfano, ambayo ni Dar es Salaam, Lindi na Mtwara kwa kutumia mapato ya ndani ya Shirika lakini zoezi litaendelea kutekelezwa katika mikoa mingine nchi nzima.
“Tuliona kusubiri fedha za wafadhili ili kuanza kutekeleza Mradi siyo jambo la busara wakati Shirika letu la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kwa sasa linafanya biashara. Hivyo tumeanza na mapato yetu ya ndani kupitia Shirika hilo.”
Akizungumzia manufaa ya Mradi huo, Waziri Kalemani alisema mtumiaji aliyeunganishiwa gesi asilia nyumbani, anapata unafuu wa asilimia 40 ikilinganishwa na gharama ya mtungi mmoja wa gesi na asilimia 35 kwa kulinganisha na gunia moja la mkaa lenye uzito wa kilo 25 hadi 50.
Alisema, Mradi utagharimu shilingi za kitanzania bilioni 8.8 kwa Dar es Salaam na shilingi bilioni 5.7 Mtwara ambapo nyumba mpya 26 zimeunganishwa na kufanya idadi yake kufikia 96 hadi sasa.
“Matarajio ni kuwa ifikapo Septemba mwaka huu, nyumba 337 ziwe zimeunganishwa katika mikoa ya Mtwara na Dar es Salaam pamoja na Taasisi za Umma zikiwemo Shule na Hospitali kufikia 10.”
Akijibu hoja mbalimbali zilizotolewa na Wabunge husika wakati wa majumuisho, Waziri pia alizungumzia hali ya mafuta nchini ambapo alisema iko vizuri kwani hadi sasa, nchi ina hifadhi ya ziada ya lita milioni 125 za mafuta ambayo yanatosha kwa matumizi ya siku 35 hadi 52.
“Ieleweke kwamba ziada hiyo hatuigusi kwani mafuta yanaendelea kuingia kila wiki. Mafuta ni usalama, hivyo kuwa na ziada inatusaidia kuhakikisha usalama wa nchi,” alifafanua.
Kuhusu Mradi wa Gesi Asilia Iliyosindikwa (LNG), alisema uko katika hatua za majadiliano ambayo yanatarajiwa kukamilika kufikia Septemba mwaka huu. Alisema, hatua itakayofuata ni ujenzi ambao utachukua takribani miaka mitano.
“Tunatarajia kutumia takribani shilingi bilioni 5.1 kuwalipa fidia wananchi watakaopisha Mradi huu.”
Waziri pia alizungumzia manufaa ya Mradi wa Bomba la Mafuta kutoka Hoima hadi Tanga, ambapo alifafanua kuwa mbali ya ajira na kodi mbalimbali, Serikali pia itanufaika kutokana na malipo yanayotokana na kiasi cha mafuta kitakachokuwa kinapitishwa kwenye bomba husika.
“Bomba hilo lina uwezo wa kupitisha mapipa 216 ya mafuta kwa siku. Sisi kama wadau tutalipwa Dola 12.2 kwa kila Pipa la mafuta litakalopita kwenye Bomba. Asimilia hizo za fedha zitaingia kwenye mapato ya Serikali,” alisisitiza Waziri.
Aidha, Waziri alieleza kuwa, Serikali ina mpango wa kuanza kuratibu uagizaji wa gesi ya mitungi kwa pamoja ili pamoja na mambo mengine, kuwasaidia wananchi kupata gesi ya uhakika na yenye gharama stahiki.
Alisema, utekelezaji wa mpango huo utahusisha pia kuhakikisha gesi ya mitungi inafikishwa hadi vijijini ili kuwasaidia wananchi kuondokana na matumizi ya kuni na mkaa.
Katika Semina hiyo ya Wabunge wa Kamati ya PIC, Mada mbalimbali ziliwasilishwa zikiwemo majukumu na madaraka ya TPDC, chimbuko la mikataba kifani ya ugawanaji mapato (MPSA), shughuli za mkondo wa juu, kati na chini pamoja na mchango na matarajio ya sekta ya mafuta na gesi.
Viongozi wengine walioshiriki Semina husika ni pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Mwinyimvua, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TPDC, Prof. Sufian Bukurura pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Kapuulya Musomba.