Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji
ya Umma (PIC), Dkt. Raphael Chegeni (katikati), akizungumza jambo wakati wa
Semina iliyoandaliwa na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kwa
Kamati hiyo kuhusu mchango wa sekta ya gesi na mafuta katika uchumi, Dodoma,
Mei 25, 2019. Kushoto ni Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani na kulia ni
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Mhandisi Kapuulya Musomba.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akizungumza wakati wa Semina
iliyoandaliwa na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kwa Kamati ya
Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) kuhusu mchango wa sekta ya gesi na
mafuta katika uchumi, Dodoma, Mei 25, 2019.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akizungumza wakati wa Semina
iliyoandaliwa na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kwa Kamati ya
Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) kuhusu mchango wa sekta ya gesi na
mafuta katika uchumi, Dodoma, Mei 25, 2019.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania
(TPDC), Mhandisi Kapuulya Musomba akiwasilisha Mada kuhusu mchango wa sekta ya
gesi na mafuta katika uchumi, wakati wa semina kwa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji
wa Mitaji ya Umma (PIC), iliyofanyika Dodoma, Mei 25, 2019.
Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), ambaye
pia ni Mbunge wa Muleba Kaskazini, Charles Mwijage akichangia hoja, wakati wa
semina kwa Wabunge wa Kamati hiyo, kuhusu mchango wa sekta ya gesi na mafuta
katika uchumi, Dodoma, Mei 25, 2019.
Sehemu ya Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma
(PIC), wakifuatilia mada mbalimbali katika Semina kuhusu mchango wa sekta ya
gesi na mafuta katika uchumi, Dodoma, Mei 25, 2019.
Sehemu ya Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma
(PIC), na wataalamu kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC),
wakifuatilia mada mbalimbali katika Semina kuhusu mchango wa sekta ya gesi na
mafuta katika uchumi, Dodoma, Mei 25, 2019.
xxxxxxxxxxxxxxxxxx
Na Veronica Simba - Dodoma
Serikali imesema Mradi wa kuunganisha gesi asilia
majumbani ni endelevu na utafanyika katika mikoa yote nchi nzima awamu kwa
awamu.
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani, alibainisha hayo jana, Mei 25,
2019 jijini Dodoma katika Semina ya Wabunge wa Kamati ya Uwekezaji wa Mitaji ya
Umma (PIC) ambayo ililenga kuwajengea uelewa kuhusu mchango wa sekta ya gesi na
mafuta katika uchumi wa nchi.
Akifafanua, Waziri aliwaeleza wabunge hao kuwa usambazaji wa gesi asilia
majumbani umeanza katika Mikoa mitatu ya mfano, ambayo ni Dar es Salaam, Lindi
na Mtwara kwa kutumia mapato ya ndani ya Shirika lakini zoezi litaendelea
kutekelezwa katika mikoa mingine nchi nzima.
“Tuliona kusubiri fedha za wafadhili ili kuanza kutekeleza Mradi siyo
jambo la busara wakati Shirika letu la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kwa
sasa linafanya biashara. Hivyo tumeanza na mapato yetu ya ndani kupitia Shirika hilo.”
Akizungumzia manufaa ya Mradi huo, Waziri Kalemani
alisema mtumiaji aliyeunganishiwa gesi asilia nyumbani, anapata unafuu wa
asilimia 40 ikilinganishwa na gharama ya mtungi mmoja wa gesi na asilimia 35
kwa kulinganisha na gunia moja la mkaa lenye uzito wa kilo 25 hadi 50.
Alisema, Mradi utagharimu shilingi za kitanzania
bilioni 8.8 kwa Dar es Salaam na shilingi bilioni 5.7 Mtwara ambapo nyumba mpya
26 zimeunganishwa na kufanya idadi yake kufikia 96 hadi sasa.
“Matarajio ni kuwa ifikapo Septemba mwaka huu, nyumba
337 ziwe zimeunganishwa katika mikoa ya Mtwara na Dar es Salaam pamoja na
Taasisi za Umma zikiwemo Shule na Hospitali kufikia 10.”
Akijibu hoja mbalimbali zilizotolewa na Wabunge husika
wakati wa majumuisho, Waziri pia alizungumzia hali ya mafuta nchini ambapo
alisema iko vizuri kwani hadi sasa, nchi ina hifadhi ya ziada ya lita milioni
125 za mafuta ambayo yanatosha kwa matumizi ya siku 35 hadi 52.
“Ieleweke kwamba ziada hiyo hatuigusi kwani mafuta
yanaendelea kuingia kila wiki. Mafuta ni usalama, hivyo kuwa na ziada
inatusaidia kuhakikisha usalama wa nchi,” alifafanua.
Kuhusu Mradi wa Gesi Asilia Iliyosindikwa (LNG),
alisema uko katika hatua za majadiliano ambayo yanatarajiwa kukamilika kufikia
Septemba mwaka huu. Alisema, hatua itakayofuata ni ujenzi ambao utachukua
takribani miaka mitano.
“Tunatarajia kutumia takribani shilingi bilioni 5.1
kuwalipa fidia wananchi watakaopisha Mradi huu.”
Waziri pia alizungumzia manufaa ya Mradi wa Bomba la
Mafuta kutoka Hoima hadi Tanga, ambapo alifafanua kuwa mbali ya ajira na kodi
mbalimbali, Serikali pia itanufaika kutokana na malipo yanayotokana na kiasi
cha mafuta kitakachokuwa kinapitishwa kwenye bomba husika.
“Bomba hilo lina uwezo wa kupitisha mapipa 216 ya
mafuta kwa siku. Sisi kama wadau tutalipwa Dola 12.2 kwa kila Pipa la mafuta
litakalopita kwenye Bomba. Asimilia hizo za fedha zitaingia kwenye mapato ya
Serikali,” alisisitiza Waziri.
Aidha, Waziri alieleza kuwa, Serikali ina mpango wa
kuanza kuratibu uagizaji wa gesi ya mitungi kwa pamoja ili pamoja na mambo
mengine, kuwasaidia wananchi kupata gesi ya uhakika na yenye gharama stahiki.
Alisema, utekelezaji wa mpango huo utahusisha pia
kuhakikisha gesi ya mitungi inafikishwa hadi vijijini ili kuwasaidia wananchi
kuondokana na matumizi ya kuni na mkaa.
Katika Semina hiyo ya Wabunge wa Kamati ya PIC, Mada
mbalimbali ziliwasilishwa zikiwemo majukumu na madaraka ya TPDC, chimbuko la
mikataba kifani ya ugawanaji mapato (MPSA), shughuli za mkondo wa juu, kati na
chini pamoja na mchango na matarajio ya sekta ya mafuta na gesi.
Viongozi wengine walioshiriki Semina husika ni pamoja
na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Mwinyimvua, Mwenyekiti wa Bodi
ya Wakurugenzi TPDC, Prof. Sufian Bukurura pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji
wa TPDC, Kapuulya Musomba.
No comments:
Post a Comment